Breaking News

Kutoka kwenye kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, Soma mambo mazito yaliyoandikwa juu ya John Okello

BY  Yericko Nyerere

Image result for john gideon okello photos
 Baada ya kuona namna mwanamapinduzi halisi, Field Marshal John Gideon Okello, alivyoondolewa Zanzibar na kupokwa mamlaka na jinsi alivyoongoza Mapinduzi ya mwaka 1964, na kuundwa kwa Serikali ya Mseto kati ya vyama vya ASP na Umma, sasa tunaona kunaibuka lengo la Karume la kuzivunja nguvu za wanaharakati na wakomunisti wa ASP walioshabihiana kimawazo na kimtazamo wa utaifa na wana-Umma Party, na hivyo kumnyima Karume usingizi wa pono katika muda mfupi wa utawala baada ya mapinduzi hayo, tofauti na matarajio ya Karume juu ya unafuu wa Muungano, hatua hiyo iliwaleta karibu zaidi wanamapinduzi hao na kumnyima zaidi usingizi kwa hofu ya kupinduliwa, akituhumiwa vikali kushindwa kuongoza na kusimamia madhumuni ya Mapinduzi yaliyopindua mapinduzi Visiwani Zanzibar.

Safari ya Abeid Krume dunia, Kuzaliwa kwake, makuzi yake, nguvu ya mamlaka ya nchi hadi kifo chake ni habari zinazosisimua na kuzaa udambwidambwi mbele ya vilindi na vilima vyote vya mioyo na fahamu za wanadamu walio hai. Safari ya Abeid Karume ni ndefu inayoanzia vilima vya Rodesia ya Kusini ama Nyasaland ama Malawi ya leo. Amani Karume baba wa Abeid Karume alizaliwa 1875 huko Kachulu nchini Malawi pembezoni mwa Ziwa Nyasa toka kabila la Sena. Akiwa na miaka 15 kwakuwa dunia haikuwa na mipaka, akasafiri kutoka Kachulu hadi Meponda na Montepuz nchini Msumbiji, na alipofikisha miaka 25 akahama kuelekea Pemba nchini Msumbiji katika kutafuta malisho mema ya kibinamu. Alikaa hapo kwa miaka michache, alipotimiza miaka 27 akasafiri kwa shughuli za uvuvi hadi Pongwe, Mudiria ya Mwera kisiwani Unguja ambako ndiko maisha yake yalikokomea na kizazi chake kukijenga hapo.
Bwana Abeid Amani Karume rais wa pili na mwenyekiti wa pili wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar baada ya kufukuzwa kwa mwanamapinduzi rais wa kwanza na mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Bwana John Gideon Okello, alizaliwa katika kitongoji cha Pongwe, Mudiria ya Mwera kisiwani Unguja tarehe 4 Agosti 1905. Karume ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya watoto watano ya Bwana Amani Karume na Bibi Amina binti Kadir (Amina Kadudu). Bwana Amani Karume na Bibi Amina Binti Kadudu walifunga ndoa huko Mwera. Bwana Abeid Amani Karume alizaliwa na ndugu wanne wa baba mmoja na mama mmoja ambao ni wanaume wawili na wanawake wawili. Lakini wote walifariki kutokana na maradhi mbalimbali na kubaki yeye peke yake.
Kwa upande wa mama mmoja, Abeid Amani Karume alizaliwa na ndugu watatu, wanawake wawili na mwanaume mmoja ambao ni Asha, Shumbana na........,.........
Kwa undani zaidi Soma Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.
Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi, na Kitabu cha Strategy: The Road to Power, vinapatikana kwa Dar es Saalam duka la House Of Wisdom, Posta, Samora, NHC House.
UJASUSI: Kitabu cha watu wote waliopevuka kiakili ni shilingi elfu themanini (80,000/=)
STRATEGY: Kitabu maalumu kwa wagombea wa urais, ubunge na udiwani, ni shilingi laki saba (700,000/=)
Nunua pia kupitia mitandao ya amazon.comebay.com au simgazeti.com
Piga simu sasa popote ulipo utaletewa...
Mawasiliano +255715865544
+255755865544
No automatic alt text available.